Utambulisho kuhusu kanisa
Church on the rock Kimana ni kanisa la kiroho linalokua kwa kasi kubwa ambalo jukumu lake kubwa ni kuunganisha jamii na KRISTO, kuhudumia jamii kiroho na kuwafikia wahitaji. Kazi kubwa ya kanisa inatoka katika agizo kuu aliloliacha YESU KRISTO ambalo linapatikana katika kitabu cha Mathayo 28:19. Katika kutimiza majukumu yake ya kulitimiza agizo kuu, kanisa limefanikiwa kuwa na vikundi mbalimbali vinavyofanya kazi kwa pamoja kuufikia ulimwengu wote na kuwapa habari njema za wokovu.Vikundi hivyo ni pamoja na kikundi cha uinjilist na umisheni, vikundi vya uimbaji(Wingu la Neema choir, Sifa Voices Ministry na Praise and worship team), vikundi rika (vijana, wazee, watoto, wamama), vikundi vya ushirika wa nyumbani ( 11 home cells) ambavyo kwa pamoja vinafanya kazi chini ya REV. Jackson Ole Mwaura
Mahali pa kulipata kanisa(LOCATION)
Kanisa linapatikana Kimana town barabara ya kuelekea Loitokitok, kabla hujatoka nje ya town ya Kimana utaona bango kubwa litakalokuelekeza ni wapi linapatikana kanisa. Pia tuko na matawi Rombo na Tikondo B Kama ukishindwa kufika unaweza kupata msaada zaidi kupitia namba hizi za mawasiliano:-
+254724925911
KARIBU USHIRIKI NASI

Safi sana
ReplyDeleteSafi sana
ReplyDelete